March 4, 2017 ligi kuu ya England baadhi ya mechi zimechezwa siku hii ya leo mechi ya mapema ni kati ya Manchester United akiwa nyumbani Old Trafford akiwakaribisha Afc Bournemouth.
Man United walitegemea mechi hii kuingia top 5 ya ligi kuu ya England ila mambo yamebadilika kwa kulazimishwa suluhu ya 1-1.
Goli la Man United limefungwa na Marcos Rojo dakika ya 23 wakati Zlatan Ibrahimovic kukosa mkwaju wa penati dakika ya 72. huku Bournemouth wakisawazisha goli kwa mkwaju wa penati kupitia kwa mchezaji wao Joshua King dakika ya 43.
Manchester United wamebaki nafasi ya sita kwa jumla ya point 49.
No comments:
Post a Comment