Manchester united yakamilisha usajili wa beki kutokea Benfica victor Lindelof mwenye miaka 22.
Kinda huyu kutokea Benfica ameenda kwa ada pauni million 30.7
Manchester united yakamilisha usajili wa beki kutokea Benfica victor Lindelof mwenye miaka 22.
Kinda huyu kutokea Benfica ameenda kwa ada pauni million 30.7
27, apr 2017 ligi ya England alimahalufu kama Premier league iliendelea baadhi ya timu zilicheza katikati ya wiki hii moja. kati ya mechi kubwa ikiyotazamwa na mashabiki wengi wa soka ni kati ya dabi ya jiji la Manchester kati ya man city akiwa nyumbani Etihad Stadium akimkaribisha Man United.
Mpaka dakika ya 90 za mchezo Man city na Man United walitoshana nguvu ya bila kufungana 0-0.
ila kuna matukio mawili yaliyojitokeza ndani ya mchezo huo.
›Tukio la kwanza, mchezaji wa Man united Fellaini kuzawadiwa kadi nyekundu dakika ya 84'.
›Tukio la pili, kipa wa Man city Bravo kupata majelaha katika dakika ya 78' na kutolewa nje kwa matubabu zaidi.
Man city akibaki kwenye nafasi yake ileile ya nne akiwa na point 65 huku akifatiwa na Man United kwa tofauti ya point moja.
Apr 23, 2017 Mbio za kumalizia ligi nchini Spain alimahalufu La Liga jumapili hii kulikua kuna mechi nne ila mechi iliyokua ikatazamwa na wapenzi wa soka duniani ni El Clasico kati ya Real Madrid akiwa nyumbani Santiago Bernabéu akiwakaribisha watani wao wa jadi Barcelona.
Madrid apokea kichapo cha goli 3-2 magoli ya Madrid yakifungwa na Casemiro dakika ya 28 pia dakika ya 77 Sergio Ramos amepigwa kadi nyekundu goli la pili likifugwa na James Rodriguez dakika ya 86.
Magoli ya Barcelona yamefungwa na Lionel Messi dakika ya 33, goli la pili likifungwa na Ivan Raktic dakika ya 73, Lionel Messi kumaliza mchezo dakika ya 90.
Barcelona wanaongoza ligi kwa point 75 sawa na Madrid kwa tofauti ya magoli pia Madrid wapo nyuma kwa mchezo mmoja.
March 4, 2017 ligi kuu ya England baadhi ya mechi zimechezwa siku hii ya leo mechi ya mapema ni kati ya Manchester United akiwa nyumbani Old Trafford akiwakaribisha Afc Bournemouth.
Man United walitegemea mechi hii kuingia top 5 ya ligi kuu ya England ila mambo yamebadilika kwa kulazimishwa suluhu ya 1-1.
Goli la Man United limefungwa na Marcos Rojo dakika ya 23 wakati Zlatan Ibrahimovic kukosa mkwaju wa penati dakika ya 72. huku Bournemouth wakisawazisha goli kwa mkwaju wa penati kupitia kwa mchezaji wao Joshua King dakika ya 43.
Manchester United wamebaki nafasi ya sita kwa jumla ya point 49.
February 26, 2017 ndio siku ya historia kwa kocha wa Man United Jose Mourinho baada ya kuchukua kikombe cha EFL Cup.
Mechi ya fainali iliyochezwa katika uwanja wa Webley ili zikutaniasha timu mbili bola Manchester United na Southampton.
Man United imeibuka washindi wa goli 3-2 magoli yote mawili ya Southampton yakifungwa na Manolo Gabbiadini katika dakika ya 45 na 49. Na magoli ya Manchester United yakifungwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 19 na dakika ya 87 huku Jesse Lingard akiifungia Man United goli la pili dakika ya 39.
Manchester United imechukua ELF Cup mala 5 huku Zlatan Ibrahimovic ndio amekua mfungaji bola wa ashindano hayo 2017 baada ya kuifungia Man United magoli 4.
Leo February 26 , 2017 La Liga imeendelea kutimua vumbi katika viwanja tofauti tofauti ila wapenzi wengi wa soka walitupia macho kwenye mechi ya Barcelona na Atletico Madrid.
Japo Barcelona imeonesha kiwango kidogo baada ya mechi iliyopata kupoteza zidi ya PSG lakini imeonesha ubola wake leo hii baada ya kupata ushindi mnono zidi ya wapinzani wao wa jadi Atletico Madrid.
Atletico Madrid akiwa nyumbani kwake Vicente Carderon akiwakalibisha Barcelona amepokea kichapo cha bao 2-1.
Magoli ya Barcelona yamefungwa na Rafinha dakika ya 64, wakati dakika ya 70 Diego Godlin akisawazisha , Lionel Messi akimaliza mchezo kwa kuifungia Barcelona goli la pili na la ushindi katika dakika 86.
Barcelona wameka juu jumla ya point 54 wakifatiwa na Real Madrid akiwa na point 52 akiwa anakipolo kimoja mkononi.
25, February 2017 kulikua na mchezo wa maludiano kati ya watani wa jadi Simba na Yanga Ligi kuu Tanzania bara katika uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Baada ya sare katika mchezo wa round ya kwanza ya 1-1. Round ya pili imechezwa hii leo na simba kuibuka washindi wa goli 2-1.
Goli la Yanga limefugwa na Simon msuva dakika ya 4 kwa mkwaju wa penati , magoli ya Simba yamefungwa na Laudit Mavugo dakika ya 66, goli la pili lilifugwa na Shiza Kichuya akitokea bechi.
Baada ya mechi hiyo Simba wamebakia kileleni kwa jumla ya point 54 huko Yanga wamebaki na point zake zilezile 49 akiwa na kiporo kimoja.