Sunday, February 26, 2017

Barcelona yamuua Atletico Madrid ugenini

Leo February 26 , 2017 La Liga imeendelea kutimua vumbi katika viwanja tofauti tofauti ila wapenzi wengi wa soka walitupia macho kwenye mechi ya Barcelona na Atletico Madrid.

Japo Barcelona imeonesha kiwango kidogo baada ya mechi iliyopata kupoteza zidi ya PSG lakini imeonesha ubola wake leo hii baada ya kupata ushindi mnono zidi ya wapinzani wao wa jadi Atletico Madrid.

Atletico Madrid akiwa nyumbani kwake Vicente Carderon akiwakalibisha Barcelona amepokea kichapo cha bao 2-1.

Magoli ya Barcelona yamefungwa na Rafinha dakika ya 64,  wakati dakika ya 70 Diego Godlin akisawazisha , Lionel Messi akimaliza mchezo kwa kuifungia Barcelona goli la pili na la ushindi katika dakika 86.

Barcelona wameka juu jumla ya point 54 wakifatiwa na Real Madrid akiwa na point 52 akiwa anakipolo kimoja mkononi.

No comments:

Post a Comment