Wednesday, February 22, 2017

Madrid apokea kichapo kikali ndani ya dakika 10 kutoka kwa Valencia

Usiku wa kuamkia leo umechezwa mechi mmoja kataka kombe la La Liga kati ya Valencia akiwa nyumbani katika uwanja wa Mestalla akiwakaribisha Real Madrid.

Mchezo umemalizika kwa Real Madrid kupokea kichapo kutoka kwa Valencia cha bao 2-1 magoli ya Valencia yakifungwa na Simone Zaza katika dakika ya 5, na dakika ya 9 Fabiani Orellana akiwapatia Valencia goli la ushindi. Goli la kufutia machozi kwa Madrid lilikifungwa na Cristiano Ronaldo katika dakika ya 44.

Real Madrid akisalia nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi akimzidi mpinzani wake Barcelona point moja lakini Barcelona akiwa mbele kwa mchezo mmoja.

No comments:

Post a Comment