![]() |
Countinho |
Thursday, January 26, 2017
Wednesday, January 25, 2017
Southampton imetangulia fainali ikimsubili mshindi kati ya Manchester united na Hull City. united anakalibishwa ugenini baada ya ushindi wa goli mbili bila.
fainali inategemea kuchezwa tarehe feb,26 mwaka huu katika uwanja wa wembley.
Monday, January 23, 2017
Rooney kuendeleza ubabe wake katika klabu ya man u
Mchezaji wa Manchester united Wayne Rooney ambaye ameitumikia klabu hiyo tangu mwaka 2014 kwa kipindi chote amefanikiwa kuifungia magoli 250 moja kati ya magoli mulwa aliyefunga zidi ya Stoke City January 21, idadi ya magoli hayo yamemfanya kuendeleza ubabe wake zidi ya mchezaji wa zamani wa Manchester united Bobby Charlton mwenye magoli 249.
Wenyeji wa AFCON kutulewa hatua ya makundi
Mchezo wa mwisho wa kundi A uliochezwa usiku wa January 22, ambao uliwakutanisha mwenyeji wa mashindano hayo Gabon aliyetoa sale na Cameroon mchezo huo ulimfanya Gabon kuaga mashindano hayo baada ya kutoa sale michezo yake mitatu na kumfanya kushika nafasi ya tatu akiwa na point Tatu huku akiambatana na Guinea Bissau aliye shikilia nafasi ya mwisho. Burkinafaso na Cameroon ndio wamewaza kufuzu atua ya robo fainali kwenye kundi A
Monday, January 16, 2017
Goli la Zlatan ramsisimua Rio Fredinand
January 15, 2017 ligi ya England zilipigwa mechi mbili ambazo zilitazamiwa na mashabiki wengi wa soka la ulaya moja kati ya hiyo mechi ni kati ya Manchester united akiwa nyumbani Old Trafford akimkalibisha mtani wake Liverpool mechi ikimalizika kwa suluhu ya 1-1 goli la Liverpool lilifungwa na kwa mkwaju wa penati katika dakika ya na dakik ya Zlatan akiisawazishia united ila goli hilo lilimsisimua mchezaji wa zamani wa Manchester United Rio Fredinand
Sevilla yaiua Real madrid 2-1
January 15, 2017 baadhi ya mechi za La Liga ziliendelea moja kati ya mechi iliyoangaliwa na wengi ni kati ya Sevilla akiwa nyumbani akimkalibisha Real Madrid.
Kipindi cha kwanza kilitoka suluhu bila kufungana lakini kwenye dakika ya 67 Madrid walipata mkwaju wa penati kupitia mshambuliaji wao Cristian Ronardo. Magoli ya Sevilla yakifungwa na Sergio Ramos akijifunga kwenye dakika ya 85 na dakika ya 90 Jovetic akiwapatia goli la pili Sevilla
Sunday, January 15, 2017
Pep Guardiola kupokea kichapo cha bao 4 bila
January 15, 2017 zilipigwa mechi mbili ambazo zilitazamiwa na mashabiki wengi wa soka la ulaya ni kati ya Manchester city akiwa ugenini kwa Everton.. Magoli ya Everton yalifungwa na Lukaku dakika ya 34',dakika ya 47 millaras akiwapatia goli la pili ,dakika ya 79 Davies akifunga goli la tatu, dakika ya 90 Lookman akimaliza mchezo kwa city kulala bao nne bila
Thursday, January 12, 2017
MSN wanefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali
Usiku wa kuamkia jana mashindano ya Copa del Rey ambopo mechi nne zilichezwa ambazo ni
Alves 1-1 Deportivo
Cordoba 1-2 Alcorcon
Villarreal 1-1 R. Sociedad
Lakini mechi iliyotazamwa na mashabiki wengi ni kati ya Barcelona akimkalibisha Athletic amboyo ilimazimika kwa Barcelona kupata ushindi mnono wa goli 3-1 magoli ya Barcelona yakifungwa na L. Suarez dakika ya 34 , dakika ya 48 Neymar akifunga kwa mkwaju wa penati , na dakika 78 free kick ya Lionel Messi. Ila goli la Athletic club lilifungwa na saborit dakika ya 51 michezo ukimalizika kwa MSN kuifikisha timu yao hatua ya robo fainali.
Diamond platnumz kutumbwiza kwenye ufunguzi wa AFCON
Mashindano ya AFRICA CUP OF NATION (AFCON) yametalajiwa kuanza hivi punde masani wa Tanzania Diamond platnumz ambaye atakwenda kuburudisha katika ufunguzi wa mashindano hayo hapo January 14, 2017 nchini Garbon Diamond platnumz ameangwa kwa kupewa bendela ya Taifa na waziri wa michezo Nape
Wednesday, January 11, 2017
Simba yaichalaza Yanga
Usiku wa January 10, 2017 ilisubuliwa mechi ya wapinzani wa jadi katika kombe la mapinduzi baada ya Azam FC kutinga fainali kwa kushinda bao 1 bila zidi ya Taifa Jang'ombe. Nusu fainali ya pili ilipigwa mishale ya saa mbili katika saa za Afrika mashariki katika uwanja wa Amaan Zanzibar. Yanga na Simba dakika 90 zilimalizika bila kufungana, hivyo ililazimika kupigwa penati ambazo zilimwezesha Simba kufuzu hatua ya fainali kwa penati 4-2 na kukutana na Azam FC January 13, 2017
Tuesday, January 10, 2017
Azam FC yamsainisha kocha mpya
Mbadala wa aliyekua kocha wa Azam FC kutokea Hispania Zeneb Hernandez, umepatikana hii leo baada ya kumsainisha kocha mpya kwa mkataba wa miezi sita Aristica Cioaba raia wa Romania mwenye umri wa miaka 45. Azam wameingia mkataba na kocha huyo leo huko katika visiwa vya Zanzibar na anategemea kuwepo kwenye mechi yao ya nusu fainali hapo badae kati ya Taifa Jang'ombe.
Cristiano Ronaldo asanda tena tuzo ya FIFA 2016
Shilikisho la soka duniani FIFA january 9,2017 lilitoa tuzo huko mjini Zurich Uswiss, watu wengi walitolea jicho tuzo ya mchezaji bora wa dunia iliyokua ikishindaniwa na Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, na Antoine Griezmann.
Ila mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia FIFA alikua ni Cristiano Ronaldo.
Sunday, January 8, 2017
Yanga apokea kichapo cha bao nne bila zidi ya Azam
January 7, 2017 mchezo wa mwisho kundi B ulichezwa katika uwanja wa Amaan Zanzibar. Azam fc iliyoonekana unasuasua katika mashindano hayo ila usiku huo wa jana Azam ilimshushia kichapo kikali Yanga cha goli 4-0 magori ya Azam FC yalifugwa na John Bocco dakika ya 2, Yahaya mohamed dakika ya 54, na dakika ya 80 Joseph muhundi, na goli la mwisho alifunga Enock Atta. Ushindi huo unamweka Azam FC nafasi ya kwanza akifatiwa na Yanga wakati zimamoto pamoja na Jamhuri wakiaga mashindano
Friday, January 6, 2017
Man city yatoa kichapo cha tano bila zidi ya westhum
FA Cup yaanza usiku kuamkia leo ilipigwa mechi kati ya westhum wakiwakalibisha Manchester city katika uwanja wa London stadium. Westhum wapokea kipigo chini ya kocha pep Guardiola cha 5 bila magoli ya man city yakifugwa na Yaya Toure dakika 33', dakika ya 42' Havard Nordtveit aliyejifunga, Sergio Aguero dakika ya 51' na John stones dakika ya 84'
Kiungo wa zamani wa Chelsea amesajiliwa na klabu ya china
2,January2017 kiungo wa zamani wa klabu ya Chelsea na Timu ya Taifa ya Brazil Oscar Emboaba amejiunga na klabu ya Shanghai SIPG ya China. kiungo huyo amesajiliwa kwa ada ya pound million 52 na kulipwa 400,000 kwa wiki.
Middlesbrough imekamilisha usajili wake
Middlesbrough imekamilisha usajili wake wa Mchezaji kutoka klabu ya
Astonvilla Rudy Gestede kwa dau la £6m amesaini mkataba wake mpaka 2020
Kipa wa Manchester united Sam Johnstone apelekwa kwa mkopo Astonvilla
Kipa wa Manchester united Sam Johnstone apelekwa kwa mkopo hapo Astonvilla mpaka mwisho wa msimu 2016/2017
Mlinda mlango wa Timu ya Taifa ya UGANDA denis Onyango atwaa Tuzo ya kipa bora CAF 2016
Denis Onyango, Mlinda mlango wa Timu ya Taifa ya UGANDA amechukua Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika wa ndani. #GloCAFAwards2016
Tetesi za Antonia Martial
Mshambuliaji hatari wa Manchester united na timu ya zamani Fc Monaco, A.k.a "NEXT THIERRY HENRY" kwa namna anavo cheza akiwa uwanjani. Mchezaji huyu Siku za hivi karibuni ameusishwa na tetesi za kwenda kujiunga na klabu ya soka nchi Uhispania "SEVILLA".
Taarifa zinasema kuna uwezekano Mkubwa wa kijana huyu kutolewa kwa mkopo hapo "January".
Hii ndio list ya wachezaji waliokamilisha usajili wao
OFFICIAL:
Kazi imeanza timu zimeanza kutoa ofa mbalimbali kwa ajili ya kujiimarisha kiusajili.
Hii ndiyo List ya Madili yaliyo kamilika mpaka sasa.
1: WILFRED NDINDI KWENDA LEICESTER.
Klabu ya Leicester imekamilisha usajiliwa wa Kiungo kutoka Klabu ya GENK Kiungo huyo amesaini mkataba wa miaka mitano.
2: JULLIAN DRAXLER KWENDA PSG.
Matajiri wa klabu ya Paris-Saint German, PSG. Wamemtambulisha Mchezaji wao mpya kutoka klabu ya WOLFSBURG. Mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka 5, Kwa ada ya €36.!
3:ALEX WITSEL KWENDA CHINA.
Klabu ya Zeint imethibitisha kuwa nyota wao "Alex Witsel" ataenda kujiunga na timu ya soka China klabu ya "Tianjin Quanjian"
4:LEONARDO PAVOLETTI KWENDA NAPOLI.
Klabu ya Napoli imenasaini ya Mchezaji "Leonardo Pavoletti" kutoka Genoa hii Leo.
5:TOMAS RINCON KWENDA JUVENTUS.
Klabu ya Juventus imemtambulisha
Kiungo wao mpya "Tomas Rincon" kutoka Katika klabu ya "Genoa". Mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka minne
6: PAUL CLEMENT NDIYE KOCHA MPYA WA SWANSEA.
Klabu ya Swansea City hii Leo Imemteua "Paul Clement" kuwa ndiye kocha mpya wa klabu hiyo Pia amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu.
Mchezaji wa KRC Genk ya Ubelgiji wilfred Ndindi asajiliwa Leicester City ya Uingereza
ONYINYE WILFRED NDINDI. Ni kiungo mpya wa Leicester city amesajaliwa toka krc GENk ya UBELGIJI. amecheza timu moja na mshambuliaji hatari Wa timu ya taifa Tanzania MBWANA SAMATTA.
NAKUPA HISTORIA FUPI YA NDINDI....
Kiungo huyu alizaliwa 16 desemba 1996 huko jijini Lagos nchini Nigeria.bado kinda kabisa. Alitumia muda wake mwingi katika kucheza soka la mitaani pamoja na watoto wenzake kabla hajaonwa na maskauti Wa klabu ya GENK.
mwaka 2015 hautasahaulika kwake kwani alifanikiwa kujiunga na klabu ya GEnk na kukabidhiwa jezi namba 25. Amecheza mechi 62 katika mashindano mbalimbali kabla hajauzwa
Amelitumikia taifa lake kuanzia soka LA vijana hadi timu ya wakubwa japo bado hawaja na namba ya kudumu kikosini Kiwango chake murua kimemshawishi kocha Claudio Ranier kutoa euro millioni 15 ili kupata huduma ya kiungo huyu maridhawa. Kwa mchezaji mweusi tena kiungo hizi ni pesa nyingi sana..
Habari za usajili Johb Obi Mikel asajiliwa huko china
Kiungo wa Chelsea Johb Obi Mikel raia wa Nigeria atimkia klabu ya Tianjin TEDA ya China baada ya kukaa Stamford Bridge miaka 10 na kutwaa makombe 11.
Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika CAF 2016
Mchezaji wa timu ya taifa ya Algeria na klabu ya Leicester City, Riyad Mahrez ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika CAF kwa mwaka 2016.
Wachezaji 11 bora zaidi barani Afrika 2016
Wachezaji 11 bora zaidi barani Afrika 2016 kwa mujibu wa CAF ndio hawa.
1. Denis Onyango (Uganda)
2. Serge Aurier ( Ivory Coast)
3. Joyce Lomalisa ( DR Congo)
4. Eric Bailly ( Ivory Coast)
5. Aymen Abdennour (Tunisia)
6. Keegan Dolly (South Africa)
7. Khama Billiat (Zimbabwe)
8. Rainford Kalaba (Zambia)
9. Pierre-Emerick Aubameyang ( Gabon)
10. Riyad Mahrez ( Algeria)
11. Sadio Mane (Senegal)
Monday, January 2, 2017
Matokeo ya ligi kuu ya England
Round ya pili ya ligi kuu ya England imeanza siku hii ya leo mechi 6 katika viwanja tofauti tofauti matokeo yapo hapo chini;
Middlesbrough 0-0 Leicester city
Everton 3-0 Southampton
Manchester city 2-1 Burney
Sunderland 2-2 Liverpool
West Bromwich 3-1 Hull City
West hum Albion 0-2 Man united
Yanga atoa kichapo cha 6 bila zidi ya Jamhuri
Michezo ya kundi B yaanza kutimua vumbi siku hii ya leo katika kombe la mapinduzi cup huko zanzibar michezo wa kwanza kati ya Azam ashinda moja kati zidi ya zimamoto.
Mchezo uliofuata ni kati Yanga na Jamhuri. Yanga akipata ushindi wa bao 6 bila ushindi huo umewafanya wawe juu katika kundi lao kwa magoli
Goli la Giroud limekua kivutio kwa mashabiki wa soko
January 1, 2017 ligi kuu ya england iliendelea kwa michezo miwili katika viwanja viwili tofauti kati ya Watford akiwa nyumbani vicarage akipokea kichapo cha goli 4 kwa 1 zidi ya Tottenham. Ila katika uwanja wa Emirates Arsenal akiwa nyumbani akipata ushindi mnene 2-0 zidi ya crystal palece magoli yakifugwa na O.Giroud katika dakika ya 17 na dakika ya 56 iwobi akifunga goli la pili. Ila goli la kwanza la Arsenal lililofungwa na mfaransa Oliver Giroud limekua kivutio kikubwa zaidi kwa wapenzi wa soka la England na kuzungumziwa sana katika mitandao ya kijamii likifananiswa na goli la mchezaji wa mancherster united Henrick mkhitaryan alilofunga zidi ya Sunderland
Arsenal kupokea kichapo kikali kutoka kwa man city
Jumapili ya December 18, 2016 Ligi kuu ya England imeendelea kutimua vumbi ilipigwa big match kati ya Manchester city zidi ya Arsenal. Manchester city akiwa nyumbani katika uwanja wake wa etihad.. Dakika ya 90 zimemalizika kwa ushindi mnono kwa man city bao 2-1.
Arsenal walipata goli la kwanza dakika ya 5 kupitia mchezaji wao Theo walcott na magoli ya Manchester city yalifungwa na leroy sane dakika ya 47 na dakika ya 71 Raheem sterling akimaiza mchezo.