Usiku wa January 10, 2017 ilisubuliwa mechi ya wapinzani wa jadi katika kombe la mapinduzi baada ya Azam FC kutinga fainali kwa kushinda bao 1 bila zidi ya Taifa Jang'ombe. Nusu fainali ya pili ilipigwa mishale ya saa mbili katika saa za Afrika mashariki katika uwanja wa Amaan Zanzibar. Yanga na Simba dakika 90 zilimalizika bila kufungana, hivyo ililazimika kupigwa penati ambazo zilimwezesha Simba kufuzu hatua ya fainali kwa penati 4-2 na kukutana na Azam FC January 13, 2017
No comments:
Post a Comment